

This article is more than 1 year old
Kutambuliwa kwa Nchi katika Kiswahili
SBS inawatambua wa Aboriginal na watu wa visiwa vya Torres Strait kama Wamiliki wa Jadi wa nchi hii, na uhusiano wao wakudumu na unao endelea na ardhi, bahari, anga na jamii.
Published 3 July 2023 8:01am
Presented by Gode Migerano
Source: SBS
Image: - (Julia Esteve/Getty Images)
Kauli ya Kutambuliwa kwa Nchi kawaida hutolewa kabla ya utambulisho au ukaribisho katika matukio mbali mbali ya umma na yakibinafsi, kama hotuba na mikutano.
Ni mbinu yakuwatambua Wamiliki wa Jadi wa nchi ambako, tukio lina fanyika.
Vipindi vya SBS Audio huanza kwa kauli ya Kutambuliwa kwa Nchi, katika lugha ya kipindi kilicho hewani.
Huwa tunafanya hivi kutambua uhusiano wa Aboriginal na watu wa visiwa vya Torres Strait na nchi, pamoja nakutoa heshima zetu kwa Wazee wakale nawa sasa.
Ni njia pia ya kutambua kuwa Australia, ni nchi ambako mamlaka ya wamiliki hayaja wahi tolewa.
Hakuna maandalizi maalum wa maneno ya Kutambuliwa kwa Nchi, na mtu yeyote anaweza toa kauli hiyo.
Hotuba ya Kukaribishwa kwa Nchi hutolewa na Wamiliki wa Jadi, au watu jamii yawa Aboriginal na visiwa vya Torres Strait ambao wamepewa ruhusa na Wamiliki wa Jadi, kuwakaribisha wageni katika nchi yao.
Huu hapa mfano wa kauli ya kutambua Nchi;
Tungependa kuwatambua Wamiliki wa Jadi wa ardhi, anga, njia za maji nakutoa heshima zetu kwa Wazee wa kale na wa sasa. Tunatoa heshima zetu kwa tamaduni kongwe zaidi inayo endelea duniani.
LISTEN TO

Acknowledgement of Country in Swahili
00:21
Learn more about the Acknowledgement of Country

How to Acknowledge Country in a meaningful way
Share